Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh.
Ridhiwani Kikwete akikata utepe kuzindua maktaba ya shule ya sekondari
ya Chalinze mjini Chalinze jana ambayo imejengwa na Kampuni ya Tanga
Cement kupitia bidhaa yake ya Simba Cement kwa kushirikiana na taasisi
ya Read International kwa gharama ya shilingi milioni 42 za kitanzania
katika kuboresha elimu jimboni humo, Mbunge huyo pia ameahidi kujenga
jiko katika shule hiyo na kuongeza kompyuta ili wanafunzi wajengewe
mzingira mazuri zaidi ya kujisomea lakini pia ameahidi kushughulikia
tatizo la wanafunzi 10 ambao wamefauru kwenda kidato cha ano na sita
lakini hawakupata nafasi ya kuchaguliwa, hivyo ameueleza uongozi wa
shule hiyo pamoja na wazazi kwamba wanafunzi hao lazima watafutiwe
nafasi ya kuendelea na shule hata kama itakuwa siyo ndani ya jimbo la
Chalinze, “Muhimu wapate nafasi ya kuendelea na elimu yao ya kidato cha
tano na sita” Alisema Mh. Ridhiwani Kikwete alimuomba mwenyekiti wa
bodi ya shule hiyo Bw. Mbwana Madeni amkabidhi majina ya wanafunzi wote
kumi ili yaanze kufanyiwa kazi mara moja.(PICHA NA KIKSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-CHALINZE)
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh
Ridhiwani Kikweteakipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya shule
ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni kabla ya kuzindua rasmi maktaba
ya shule hiyo, Katikati ni Emma Lyu kutoka taasisi ya Read International
na kushoto ni Raquel Araya kutoka Taasisi ya Read International pia.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh
Ridhiwani Kikwete akionyeshwa vitabu mbalimbali vilivyopo katika maktaba
ya shule ya sekondari ya Chalinze na Najma Juma kutoka Chuo Kikuuu cha
Dar es salaam UDSM ambaye anafanya kazi za kujitolea katika taasisi ya
Read Internional.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh
Ridhiwani Kikweteakiangalia kitabu wakati akikagua maktaba hiyo kulia
kwake ni Najma Juma wa Read International.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh
Ridhiwani Kikweteakiweka alama za kiganja chake kama kumbukumbu wakati
alipozindua maktaba hiyo jana kwenye shule ya sekondari ya Chalinze.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh
Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo wakati Mwenyekiti wa bodi ya shule
ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni alipokuwa akisoma risala yake
mbele ya mbunge huyo, kutoka kulia ni Raquel Araya kutoa taasisi ya Read
International na mkuu wa ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh
Ridhiwani Kikwetea akizungumza na wanafunzi wa sule ya sekondari ya
Chalinze pamoja na walimu mara baada ya kuzindua maktaba katika shule
hiyo jana kushoto ni Mbwana Madeni mwenyekiti wa bodi ya shule, na
kutoka kulia ni Raquel Araya kutoka Read International na mkuu wa ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh
Ridhiwani Kikwetea akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kuzindua maktaba hiyo kushoto ni mdau wa masuala ya habari Dk Fadhil
Kabujanta wa Fadhaget Sanitarium Clinic ya Mbezi Africana jijini dar es
salaam.
Meneja masoko wa Simba Cement
Yasin Hussein akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa
Maktaba ya shule hiyo iliyojengwa na Kampuni hiyo gharama yake ikiwa ni
shilingi milioni 42 za kitanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni