Alhamisi, 28 Agosti 2014

DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA SARATANI YA MATITI KUTOKA INDIA ATUA NCHINI, KESHO KUENDESHA MHADHARA HOTELI YA PROTEA COURT YARD SEAVIEW JIJINI DAR ES SALAAM


 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akimtambulisha kwa madaktari (hawapo pichani), Daktari Bingwa wa magonjwa ya saratani ya matiti, Profesa Anthony Pais, kutoka Bangorole India,  Dar es Salaam jana. Daktari huyo kesho jioni anatarajia kufanya mhadhara na madaktari wa Kitanzania na wadau wa sekta ya afya kujadili ugonjwa huo katika Hoteli ya Protea Court Yard. Daktari huyo yupo nchini kwa mwaliko maalumu wa mshauri huyo wa Kimataifa.
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akiwa na daktari huyo (katikati), Kushototo ni Mama Benedicta Rugemalira. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Profesa Anthony Pais (katikati), akizungumza na madaktari wa Tanzania. Kushoto ni Dk.Maleare na Dk. Fredy
 Profesa Anthony Pais (kulia), akizungumza na madaktari wa Tanzania.
Wadau wa sekta ya Afya wakiagana na daktari huyo nyumbani kwa Mshauri wa Kujitegemea wa Kimataifa, James Rugemalira Makongo Juu jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Tanzania
DAKTARI Bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti , Profesa Anthony Pais, kutoka Bangorole nchini India kesho Agosti 28, 2014  anatarajia kutoa muhadhara kuhusu ugonjwa huo.

Akizungumza na Mtandao wa www.habari za jamii.com. Dar es Salaam leo Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira alisema ujio wa daktari huyo hapa nchini ni fursa kwa watanzania kutokana na changamoto kubwa iliyopo kuhusu ugonjwa huo.

"Daktari huyu amebobea katika ugonjwa wa saratani ya matiti na amefanya operesheni nyingi za ugonjwa huo ni wakati mzuri kwetu kwenda kumsikiliza kesho jioni Hoteli ya  Protea Court Yard" alisema Rugemalira.

Alisema kesho daktari huyo atatoa mhadhara kwa madaktari wa kitanzania na wadau wa sekta ya afya kuhusu ugonjwa huo na jinsi ya kukabiliana nao.

Rugemalira alisema daktari huyo atakuwepo nchini kwa siku kadhaa na leo alitembea Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Taasisi ya Kansa ya Ocean Road na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Daktari huyo yupo nchini kwa mwaliko maalumu wa mshauri huyo wa kimataifa ili kuona namna ya kusaidia tatizo hilo. 

RAIS KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA UZINDUZI WA PROGRAMU YA UIMARISHAJI WA MIPAKA YA KIMATAIFA MKOANI KAGERA



  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi alipowasili eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi baada ya kuwasili eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi kuhudhuria  sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi baada ya kuwasili eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi kuhudhuria  sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Wengine ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Balozi wa Burundi nchini Tanzania Mhe Issa Ntambuka


 Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi akisalimiana na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospeter Muhongo  eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi kuhudhuria  sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.

 Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi akisalimiana na baadhi ya Watanzania walikuwepo  eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi kuhudhuria  sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. 


Sehemu ya umati wa wananchi wa Tanzania na Burundi kwenye sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014

Jumatano, 27 Agosti 2014

MAELFU YA WANANCHI WAMLAKI RAIS KIKWETE GAIRO, KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO


 Rais Jakaya Kikwete akilakiwa na maelfu ya wananchi alipowasili kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014

 Mbunge wa Gairo Mhe. Ahmed Mabhut Shabiby akimkaribisha Rais Kikwete kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014
  Rais Kikwete akihutubia umati wa maelfu ya wananchi waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014
Rais Kikwete akiawaaga wananchi waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye  mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014

PICHA NA IKULU

KINANA AKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI


 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA )Nicholaus Mgaya akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili kwenye Makao Makuu ya TUCTA kwa mazungumzo na Viongozi wa vyama vya wafanyakazi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanawake,Jinsia na Watoto (TUCTA) Siham Ahmed kabla ya kuanza kwa mazungumzo baina ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi.
  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA )Nicholaus Mgaya akizungumza wakati wa kikao cha Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ukumbi wa mikutano TUCTA.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumzwa kwenye kikao na Viongozi wa Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania.
 Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) Erasto Kihwele akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
(Picha na Adam H.Mzee)

Jumatatu, 25 Agosti 2014

WABUNGE WA CCM WAFANYA MKUTANO WA HADHARA MTERA JIMBO LA DODOMA

IMG-20140824-WA0005
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi katika kijiji Iringa Mvumi Jimbo la Mtera mkoani Dodoma ambapo Chama cha mapinduzi kimeendelea kuuelimisha umma juu ya masuala ya Maendeleo, utekelezaji wa ilani, maandalizi ya uchaguzi wa serikali za vijiji na mitaa, bunge la katiba na mambo yanayohusu maendeleo ya katika vijiji na wilaya zetu. Pia kuwakumbusha juu ya thamani ya muungano wetu na vipengele muhimu vinavyojadiliwa ndani ya katiba.
IMG-20140824-WA0006
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiendelea kutema cheche katika mkutano huo.
IMG-20140824-WA0007
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo ukiwasikiliza wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya muungano ya Tanzania waliokuwa wanahutubia katika mkutano huo.
IMG-20140824-WA0008
Mbumge wa ji,bo la Sikonge Mh. Said Mkumba akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
IMG-20140824-WA0010
Wananchi wakisikiliza kwa makini Mbunge wa Chalnze Ridhiwani Kikwete alipokuwa akiwahutubia
IMG-20140824-WA0011
Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akiwahutubia wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Iringa Mvumi mkoani Dodoma.
IMG-20140824-WA0012
Mbunge wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera , Asumpta Mshana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Iringa jimbo la Mtera jana nyuma ni mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde
IMG-20140824-WA0013
Baadhi ya wananchi wakiwa wamekaa kwenye mapaa y nyumba huku wakifuatilia kutano huo.
IMG-20140824-WA0014
Umati wa wananchi aliohudhuria katika mkutano huo.
IMG-20140824-WA0015
Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akiwahutubia wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Iringa Mvumi mkoani Dodoma.
IMG-20140824-WA0017
Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akipanda jukwaani kuwahutubia wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Iringa Mvumi mkoani Dodoma baada ya mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete kuwahutubia.
IMG-20140824-WA0019 IMG-20140824-WA0020
Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akiendelea kutema cheche mbele ya wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Iringa Mvumi mkoani Dodoma.

MWIGULU NCHEMBA ASITISHA SAFARI KWA MUDA,AOKOA MAJERUHI NA KUTOA HUDUMA YA KWANZA


Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Kondakta wa Gali lililopata ajali mara baada ya Kumnasua kwenye roli hilo.Kijana anaonekana kuuguria maumivu makali kwenye Mkono.Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa Kondakta wakati Roli hilo likianguka na baadae kuinuka kutokana na kugonga Ukuta pembezoni mwa Barabara ya Iringa-Morogoro.Mh:Mwigulu Nchemba akitoka huduma ya Kwanza kwa Majeruhi wa ajali hiyo.Mh:Mwigulu Nchemba akiendelea kutoa huduma ya kwanza kwa Majeruhi kabla  ya kumkimbiza kwenda hospitali ya WIlaya ya Mikumi.
 
Na.Festo Sanga.
 
Naibu waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mh:Mwigulu Nchemba jana alifanya jambo kubwa na lakibinadamu kwa kuamua kusitisha safari yake kwa muda akielekea Iringa iliasaidi Majeruhi wa ajali ya Roli Kubwa lililokuwa likitokea Dsm kuelekea Barabara ya Iringa.
Ajali hiyo ambayo ilitokea mbele ya Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa nyuma ya Roli hilo kabla ya Kugonga Ukuta na Kuanguka haikuleta madhara makubwa.
Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ni mara kadhaa amekuwa akisaidia kuokoa majeruhi kwenye ajali anapokutana nazo barabarani,hata kwenye ajali hii alilazimika kuhakikisha majeruhi wanaokolewa na kukimbizwa Hospitali kabla ya hatua kubwa zaidi za Hospitali kuendelea,Katika ajali hiyo Mh:Mwigulu Nchemba alitumia Boksi lake la Msalaba Mwekundu(First Aid Kit) kuhudumia majeruhi hao iliwasitoke sana Damu.
Wananchi na Madreva waliopata kusimama kwenye ajali hiyo,Walimpongea sana Mh:Mwigulu Nchemba kwa namna alivyosaidia kuokoa Watanzania wenzake kwenye ajali hiyo,Wengi walisikika wakiomba Viongozi wengine waige mifano hii ya Mwigulu ya Kusimama na kuhudumia wahanga wa ajali,Kwa sababu imekuwa ikitokea Viongozi wanapoona ajali hawasimami kwa madai wanawahi ratiba za kazi zao.

MWIGULU NCHEMBA ALIVYOMSIMIKA KAMANDA WA UVCCM IRINGA-SALIM ASAS

ABaada ya Kuingia Iringa Mjini,Mh:Mwigulu Nchemba akaamua kuingia Mtaani kutembelea Matawi ya chama na Kuzungumza na Wananchi.Hapa Msafara wake ukiwa soko la Mitumba Iringa Mjini,Vijana wa CCM Iringa Mjini wakiwa mitaani Iringa Mjini.Chipukizi wa Chama Cha Mapindizi Iringa Mjini wakiwa tayari kwa Kumpokea Mgeni Rasmi Mh:Mwigulu Nchemba.Mh:mwigulu akipewa mapokezi na chipukizi wa Chama cha Mapinduzi Iringa Mjini.Msafara wa Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ukielekea Viwanja vya Mkutano.Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mwigulu Nchemba akiingia Viwanja vya Mwembetogwa Iringa Mjini tayari kwa Kumsimika Kamanda wa UVCCM Ndugu Salim Asas.Vijana wa Chama cha Mapinduzi Iringa wakifikisha Ujumbe wao kwa Watanzania.Kiongozi wa Madereva Bodaboda na Bajaji Iringa Mjini akisalimiana na Mh:mwigulu Nchemba na Kupongezwa namna anavyosimamia Uendeshaji wa Bajaji na Bodaboda Iringa Mjini.Naibu Katibu Mkuu CCM Bara akielekea Kupandwa Jukwaani tayari kwa Kuzungumza na Wakazi wa Iringa Mjini.
 Comrade Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi.Mh:Mwigulu Nchemba akisisitiza Umoja ndani ya Chama na Jumuia zake.Sehemu ya Mamia ya Wananchi waliofurika Uwanja wa Mwembetogwa kushuhudia zoezi la Kuapishwa kwa Kamanda wa UVCCM Ndugu.Salim Asas.Mwigulu Nchemba akzungumza na Wananchi waliofurika uwanja wa Mwembetogwa namna  Wizara yake ilivyoanza mikakati ya Kuhakikisha Fedha za Watanzania zinatumika ipasavyo kwenye kazi za Maendeleo,Pia lisisitiza Kubana matumizi serikalini ndio kipaumbele cha Ofisi yake kwa wakati wote wa Utendaji kazi wake.Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Comrade Mwigulu Nchemba akipata picha ya pamoja na Kamanda wa UVCCM Iringa Ndugu.Salim Asas.Katikati ni Mwenyekiti wa CCM MKoa wa Iringa Bi.Jesca Mtasavangu.Baadae Mh:Mwigulu Nchemba alitawazwa kuwa Chief wa Kihehe kama Unavyomuona ndani ya Vazi la Kichifu.
Mh:Mwigulu Nchemba akiwaaga Wananchi waliofika kwenye Shughuli ya Kusimikwa kwa Kamanda wa UVCCM Iringa.
Picha/Maelezo na Festo Sanga.