Mbunge
wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete na Diwania wa Kata ya Bwilingu Bw.
Ahmed Nasser wakiwa wamelala kwenye moja ya Vitanda 267 vilivyotolewa na
mbunge huyo katika shule mbalimbali za sekondari kwa jimbo zima la
Chalinze wakati wa makabidhiano yaliyofanyika kwenye shule ya sekondari
ya Lugoba jana, Shule ambazo zimepewa vitanda hivyo ni shule ya
sekondari Chalinze 50, Moleto Lugoba 50, Mandera 25, Talawanda 24,
Kiwangwa 50, Lugoba 38 na Kikaro 30.
katika
hatua hiyo Mh. Ridhiwania pia amepiga hatua kwa kutekeleza mambo
mbalimbali aliyoahidi wakati wa kampeni zake. Katika utekelezaji huo
ametoa Baiskeli 10 kwa walemavu, Miwani na mafuta kwa Maalbino, Jezi
pea 100 kwa ajili ya mbunge Cup mashindano ambayo yataanza baada ya
mwezi mtukufu wa Ramadhan, Visima 3 kata ya Kibindu, na 16 kwa shule
zote za sekondari jimbo zima kila shule kisima kimoja kitachimbwa.
Ametoa Transforma kubwa ya umeme kata ya Lugoba na kumaliza kabisa
tatizo la umeme katika kata hiyo, Kwa upande wa barabara amesema mvua
zimekwisha hivyo barabara zote za jimbo hilo ambazo ziliharibwa na
kutopitika sasa zitafunguliwa baada ya kupatikana kwa mdau ambaye atatoa
mashine (Mitambo)za kukarabati barabara na mafuta yapo ya kutosha
kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kabla ya kuanza tena kwa mvua za
masika ili kuzinfungua upya.
Mh. Ridhiwani pia ametoa mipira kwa shule za Msingi jimboni humo,,
ametoa Microscope kwa Zahanati ya kanisa Lugoba. na atajenga darasa 1
shule ya msingi Kiwangwa.
Wengine katika picha kulia ni Abukbakary Mlawa Meneja Uhusiano wa
kampuni ya Mamba Cement ambayo ndiyo iliyotoa vitanda hivyo na kushoto
ni Diwani wa Kata ya Lugoba Bi Rehema Mwene.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-LUGOBA)
Mbunge
wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya
Mamba ment ambayo ndiyo iliyotoa vitanda hivyo wakivikabidhi kwa Diwani
wa kata ya Bwilingu Bw. Ahmde Nasser na Mwalimu Mkuu wa Shule ya
sekondari Chalinze Bw. Emmanuel Kahabi katika makabidhiano yaliyofanyika
kwenye shule ya sekondari ya Lugoba.
Mbunge
wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi vitanda Mkuu wa shule ya
seondari ya Sekondari ya Mandera Bi. Rose Jumila, kushoto ni Diwania wa
Viti maalum kata ya Msoga Bi. Maria raban Moreto.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lugoba wakipiga pichya pamoja mbele ya vitanda hivyo kwa niaba ya wenzao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni